Mfahamu Angel Benard.
- Gospo Daily Tz
- Jun 24, 2017
- 1 min read
Wengi wanamfahamu Angel Benard kama mwimbaji wa kike wa nyimbo za injili nchini Tanzania.Ameonekana kuimba Modern New Gospel kwa muziki wake wa injili na mtindo anaoutumia katika kuimba mfano mtindo wa Rege kwenye wimbo wake wa Need you To Reign.Alizaliwa Tarehe 26-06-1989.Yeye ni mtoto wa tatu kati ya sita katika familia yao.Alianza kuimba akiwa na miaka 6 kwenye Kanisa Katoliki la Tabata Kwenye kwaya kuu.Alihitimu chuo kikuu cha UDSM baada ya kuhitimu elimu yake ya msingi na sekondari.Alirekodi mara ya kwanza mwaka 2006 kama mwimbaji wa bongo flavor ila baadae akakata shauri na kuimba Muziki wa Injili. 2008 na 2010 alirekodi album ziitwazo Yote Alimaliza na Nitakwabudu milele.Pia ana album yake ya hivi karibuni katika miaka ya nyuma iitwayo New Day.Ni mke na pia ni mama.Amefanya collabo za muziki wa Injili na wasanii wa nje ya Tanzania Kama Mercy Masika Muguro katika Wimbo wa Huyu Yesu.Anafahamika sana kwa wimbo wake wa Salama,Mungu NilInde alioimba na Shedrack Robert.Yupo pia katika vikundi au band za injili kama Glorious Celebration na Whispers Band.Amekuwa ni INSPIRATION kubwa kwa wanadada na wakaka pia kama Rogate Kalengo amabaye alishafanya naye collabo ya Jukwaani.Muda si mrefu atauachia wimbo wake wa SITEKETEI.
Comments