Kusonga Mbele
- Brian Peter Linus
- Jun 29, 2017
- 1 min read
Yesu asifiwe mpendwa, Leo tumekuja na mada ya kutiana moyo katika maisha ya kiroho na kimwili kama Kichwa cha habari kisemavyo KUSONGA MBELE. Watu wengi katika maisha tumekuwa tukiona ugumu katika mambo yetu baada ya kukatishwa moyo na ndugu na marafiki pia kuwa huwezi lakini haujajaribu hiko kitu na kujitathmini kuwa unaweza.Tumekuwa sana ''controlled'' na maneno ya watu na mitazamo yao juu yetu.Tumewafanya watu kuwa Miungu yetu zaidi ya MUNGU baba aliyeko juu mbinguni.Hakuna Mtu alyeumbwa duniani kwa kusudi la kushindwa bali kufanikiwa siku zote kwani,''BWANA HUTUWAZIA MEMA NA SIO MABAYA.''Jiamini na siku zote ujiwekee mtazamo chanya katika maisha yako. Na tunaposhindwa tusikate tama kwani tuna fursa zaidi za kuweza kujaribu tena.Tumejawa fursa katika mazingira yetu.Jiamini,Weka mikakati,Tekeleza leo na sio kesho.Leo Kwa jinsi Bwana alivyonigusa nimeona nishare nae neno hili.Daima Tujiongeze nakuachia neno zaidi kutoka kwa Christina Shusho juu ya Kujiongeza kimaisha.UBARIKIWE.
Commentaires